Gazeti la Risasi la leo limeripoti kuwa Mataa wa bongo movies ambao ni mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kugombana baada ya Aunt ‘kuposti’ kwenye ukurasa wake wa Instagram tangazo lililohusiana na pati ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ iliyofanyika Mlimani City jijini Dar wikiendi iliyopita.
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao wa sinema za Kibongo, baada ya
Aunt kuposti tangazo hilo akiwalaumu watu wa mtandao wa huduma za simu
waliomtumia ndipo Wema akaona na kuja juu.
Ilielezwa
kwamba baada ya Aunt kutupia picha ya tangazo hilo, Wema alichukizwa na
kitendo hicho huku akimuona Aunt kuwa amemsaliti.
Ilisemekana kwamba katika utetezi wake, Aunt hakupendezwa na tangazo hilo alilotumiwa na mtandao huo wa simu.
“Wema
alivyoona alichukia na kusema Aunt alikuwa akimsaliti na alitumia
tangazo lile kijanja kwa ajili ya kuwatangazia watu kuhusu pati ya Zari
wakati anajua kabisa kuwa Wema hazipandi na Zari kwa sababu anatoka na
aliyekuwa mchumba’ke (Diamond),” kilisema chanzo hicho.
Katika
sakata hilo, kuna watu ambao waliona Aunt hakuwa na kosa lakini wapo
walioona hakuwa sahihi, jambo ambalo lilichochea ugomvi wao huku
wakidaiwa kukesha wakitukanana.
Gazeti
hilo lilipozungumza na Aunt kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea
akisema kuwa hakuwa na maana mbaya kuposti tangazo hilo lakini kila mtu
ana mtazamo wake.
“Mimi
sikumaanisha chochote kibaya kuhusu hilo tangazo na wala sikujua kama
kuna mtu anaweza akalichukulia tofauti kabisa na hapo na mimi ndiyo
nashindwa cha kuzungumza,” alisema Aunt.
Alipopigiwa Wema simu yake iliita bila kupokelewa.
Post a Comment