
Wafanyakazi
kutoka Taasisi mbali mbali umma na binafsi mkoa wa Kigoma, wakiwa
wamejumuika pamoja kwenye sherehe za Mei Mosi kwenye viwanja vya Mwanga
Community Center.
SHIRIKISHO
la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), mkoani Kigoma,
wameitaka Serikali ipunguze kodi ya mishahara na kuwa chini ya asilimia
10%, kudhibiti mfumo wa bei sambamba na kupandisha mishahara ya
wafanyakazi ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
Katika
risala yao kwenye sherehe za Mei Mosi ambayo ilieleza changamoto
zinazowakabili, wafanyakazi wa mkoa wa Kigoma walisema kuwa mishahara ya
wafanyakazi ni midogo na kodi ni kubwa ukilinganisha na hali halisi ya
maisha ya sasa.
Aidha
walieleza kuwa upungufu mkubwa wa wafanyakazi kwenye maeneo mengi ni
changamoto kwa wafanyakazi waliopo na baadhi ya viongozi wa kisiasa
kuingilia majukumu ya wafanyakazi kinyume na kanuni na sheria.
“Baadhi
ya viongozi wa kuchaguliwa wamekuwa wakiwaamuru waajiri hasa
wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na Manispaa kuwahamisha,
kuwasimamisha kazi, kuwafukuza kazi na kuwafungulia mashitaka
wafanyakazi bila sababu zozote za msingi,”ilieleza sehemu ya risala
hiyo.
Mbali
na hayo wafanyakazi mkoni Kigoma pia wameainisha mambo mbali mbali
ambayo kama yatatekelezwa changamoto za wafanyakazi ikiwemo gharama
kubwa za maisha zitapungua.
Baadhi
ya mambo hayo ni kuwataka waajiri wafunge mikataba ya hali bora na
vyama vya vya wafanyakazi kwa niaba ya wafanyakazi kwa lengo la
kuboresha mishahara na maslahi mengine ya kazi na mikataba hiyo
itekelezwe na kuheshimiwa.
Pia
wameitaka serikali na waajiri binafsi kuwaendeleza waajiriwa wao
kielimu ili waendane na zama hizi za sayansi na teknolojia pamoja na
kuondoa vikwazo kwa wafanyakazi wanaopata fursa ya kwenda kujiendeleza
na serikali kuwakumbusha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwachukulia hatua
waajiri wasiopeleka michango ya waajiriwa wao kwenye mifuko husika.
Akiongea
kwenye maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu
Issa Machibya, aliahidi kushirikiana na waajiri na mamlaka zinazohusika
kushughulikia masuala yote yaliyoelezwa na wafanyakazi hao.
Kulingana
na ripoti ya Global Tax Comparison ya Benki ya Dunia mwaka 2014,
wafanyakazi wa Tanzania wanaumizwa sana katika kodi kuliko wafanyakazi
wa nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo wastani wa kodi kwa mfanyakazi wa Tanzania ni
asilimia 18%, Uganda asilimia 11%, Kenya asilimia 6.8, Burundi asilimia
10.3 na Rwanda ni asilimia 5.6%.
Wastani
wa kodi ya mfanyakazi duniani kwa mujibu wa ripoti hiyo ni asilimia
16.2%. kwa takwimu hizo sio tu kwamba wastani wa kodi ya mfanyakazi wa
Tanzania ni kubwa kuliko nyingine Afrika Mashariki, bali ni zaidi ya
wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani.
Kwa
maoni ya wananzuoni kodi ya mshahara wa mfanyakazi inapaswa kushuka kwa
asilimia 50%, yaani itoke kuwa asilimia 18% -9% kwa wastani wa kuanzia,
lakini kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), mwaka
jana ni kwamba kama watashusha kodi hiyo kutoka 18%-9%, watapoteza
mapato ya kiasi cha shilingi 704 bilioni.
Maoni
ya wananzuoni ni kwamba mapato hayo yanaweza kufidiwa kwa kutekeleza
sheria ya kodi ya majengo ambayo mpaka sasa utekelezaji wake ni asilimia
3% ambapo shilingi 25 bilioni hukusanywa, na hiyo ina maana kuwa kama
sheria hiyo itatekelezwa kwa asilimia 100% zaidi ya shilingi 800 bilioni
zitakusanywa.
Tazama matukio mbali mbali ya sherehe za Mei Mosi katika picha:

Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya, akikabidhi
zawadi mbali mbali kwa wafanyakazi hodari wakati wa sherehe za Mei Mosi.
Mfanyakazi Bora wa TANESCO Kigoma Mjini Akipokea Zawadiyake ya TV aina ya Samsung Nchi 32,
Mfanyakazi
Bora wa TPB (Tanzania Post Bank) Mr.Kafulila Malongo Akipokea Zawadi
toka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,ambapo alipewa Hundi ya Tzs
200,000/= Pamoja na Cheti cha Mfanyakazi Bora wa Mwaka 2015,
Kabla
ya Utowaji Zawadi Kulitanguliwa na Michezo Mbalimbali Kama Vile
Kukimbiza Kuku,Ngoma za Asili,Uvutaji Kamba N.k,hapa Manesi
wakishangilia ushindi baada ya kupambanishwa na Waalimu wa jinsia (Ke)
bila waalimu hao kutokea
Muongozaji wa Tukio hili Mwalimu Amon Gwahula akitangaza ushindi kwa manesi hao
pia
mchezo wa uvutaji Kamba ulifanywa na kikundi kingine cha wanaume ambapo
walihusishwa Wanaume Wafanyakazi wa Bandari (TPA) kama unavyowaona hapa
na wafanyakazi wa Tanesco Kigoma Mjini
Kushoto ni wafanyakazi wa Tanesco Wakichuana na Wafanyakazi wa Bandari Kigoma
wakijiandaa kuvuta Kamba
Wafanyakazi wa TANESCO Kigoma wakishangilia ushindi
Taswira meza kuu
pia mchezo wa kukimbiza kuku ulikuwepo
baadhi ya wafanyakazi wa meza kuu wakishangilia jambo
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na wanamkutano (Hawapo Pichani)
baadhi ya Vyombo vya Usafiri Vilivyokuwepo eneo la tukio
Sehemu Walipoketi Wafanyakazi wa Shilika la Nyumba la Taifa (NHC)-
michezo ikichukua nafasiyake
vijana wa Sarakasi toka JKT Kanembwa
Vijana wa Ngoma za Asili toka JKT wakisherehesha Mkutano


Post a Comment