Home
»
BURUDANI
»
MICHEZO
» Yanga imethibitisha mkali huyu wa soka anaondoka… nani atachukua nafasi yake?

Ni siku kadhaa zimepita toka taarifa za mshambuliaji wa kimataifa wa
Yanga Kpah Sherman zitoke kuwa anatakiwa na klabu moja inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini na kwa uhakika
millardayo.com ilimtafuta katibu mkuu wa
Yanga Dk. Jonas Benedict Tiboroha.
Tiboroha kathibitisha kuuzwa kwa
Kpah Sherman kwenda katika klabu ya
Mpulanga Black Aces kwa ada ya uhamisho ambayo haijwekwa bayana, ila mshahara amekiri atalipwa mara tatu ya aliokuwa analipwa
Yanga, hata hivyo
Tiboroha alithibitisha kutafutwa kwa mbadala wa
Sherman na ukanda anaotokea.
“Ni
kweli Kpah Sherman hivi ninavyo ongea na wewe, nilikuwa naongea na
agent wake kwamba amepata visa ya kuingia South Afrika kwa hiyo
ataondoka leo kwenda huko kwa ajili ya kufanya test za afya ambayo
kawaida huwa ni mchakato kabla ya mchezaji kusajiliwa kuingia timu
yoyote kwa uhamisho wa kimataifa, ataondoka jioni anakwenda katika timu
moja inaitwa Mpulanga Black Aces”>>> Tiboroha
”
Ila kabla sijasema mbadala na sijui kama nitakwambia sasa hivi kwa
sababu bado tupo katika hatua za mwanzo za maongezi hatujafikia
Conclusion, kwa wenzetu wanaojua sheria sio kama sisi tunaingia mtaani
hujaongea na klabu unaanza kusikia Yanga imemsajili fulani”>>>Tiboroha
“Nataka
nikwambie tu, tuna mchezaji ambaye tupo katika maongezi naye atakuwa
mbadala wa Kpah Sherman tutakapokuwa tumekubaliana na klabu yake pamoja
na yeye mchezaji tutakuja public, anyway labda niwe wazi zaidi wako
wawili mmoja anatoka Afrika Magharibi mmoja anatoka Afrika
Mashariki”>>>Tiboroha
Post a Comment