Nahodha Bayern Munich Philipp Lahm, amezungumzia tetesi za usajili zinahusu wachezaji kutoka kwenye klabu yake ya Bayern Munich. Baada ya Bastian Schweinsteiger kwenda Manchester United, sasa taarifa mchezaji Thomas Müller anaweza kuondoka Allianz Arena msimu.

Ripoti nchini Ujerumani zinasema kwamba Man United imeandaa ofa nzito kwa ajili ya Muller, taarifa zilizomfanya Lahm Kuongelea tetesi hizo za usajili.
“Kuondoka kwake sio uamuzi wangu, vitu vinatokea haraka sana katika soka. Siwezi kuwahakikishia kwamba Thomas Muller anaweza kuendelea kubaki nasi.” – Alisema Lahm wakati mkutano wa waandishi wa habari huko Shanghai China.

Post a Comment