Kama wewe ni shabiki wa muziki wa Africa
unaweza kuwa na hamu ya kufahamu ni single gani ambayo iko juu kwenye
chati za muziki huu duniani…. kwa sababu kazi yangu ni kukusogezea zote
muhimu, nakusogezea na hii kwamba kwa wiki hii ya pili ‘Nana’ video ya
ya Diamond Platnumz kupitia kituo cha Trace TV ya Ufaransa bado
imeshika namba 1.
Mbali na video hiyo kuchezwa kama namba 1 kwenye kituo hicho cha Trace TV, Diamond Platnumz
ana sababu nyingine ya kufurahi mafanikio ya kuwa msanii wa kwanza wa
Tanzania kupitia video yake ‘Nana’ kufikisha views milioni 2 tangu
iwekwe May 29, 2015.
Hizi ndio video za Africa zilizoshika Top 9 kwenye kituo cha Trace TV ikiwemo ya Diamond Plantumz.
8.Iyanya & Diamond – Nakupenda
7.Timaya ft Phyno & Deettii – Gbagam
6.Yemi Alade – Taking Over Me ft Phyno
5.Wiz Kid – Expensive Shit
4.Davido & Meek Mill – Fans MI
3.Runtown ft Uhuru – The Banger
2.Alamide – Bobo
1.Diamond Platnumz ft Mr Flavour – Nana


Post a Comment