Stori kubwakubwa tayari ziko mtaani mtu wangu, una chochote kimepita leo Jumatatu July 20 2015? Basi hizi ni baadhi ya stori zenye uzito zaidi.
Mchakato wa kupitisha Wabunge na Madiwani washika kasi CHADEMA, Waziri MkuuMizengo Pinda amesema Ubunge haitaji tena.
Waandishi wa habari wajitosa kugombea Ubunge kupitia Vyama tofauti, yumo Jerry Muro, Abdallah Majura na wengine, wadau wa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassawajitosa tena kugombea Ubunge… iko stori ya Prof. Ibrahim Lipumba kuiyumbishaUKAWA, Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya atangaza kutogombea tena Ubunge kupitia CCM.
Mbunge wa Kahama James Lembeli nae asema hatogombea Ubunge wa Jimbo hilo tena kupitia CCM, nyingine kutoka Njomba inahusu wazee 300 kumchukulia fomu Filikunjombe ya Kugombea Ubunge… Kwenye michezo pia kuna iliyoandikwa kwamba sifa za magazeti zimeilevya Yanga…

Post a Comment