
Kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na ugomvi wa Lil Wayne na Birdman, tukasikia kuwa Lil Wayne anataka kuondoka Cash Money Records kwasababu Birdman hataki kumlipa hela yake.
Tukasikia ugomvi umefikishwa Mahakamani na Lil Wayne amesisitiza kuwa ataondoka na wasanii aliokuja nao, Nicki Minaj na Drake kama Birdman hatamlipa pesa anazomdai…Lil Wayne anataka dola mil. 51 (Bil 102 za Tz).
Birdman kaamua kumuita radio personality Angie Martinez nyumbani kwake Miami kufanya nae interview kuhusu ugomvi huu, Birdman alikuwa na haya ya kusema…
>>> Lil Wayne ni mwanangu, haijalishi kumetokea nini…nataka afanye maamuzi kwa faida na maslahi yake, nilikutana na Wayne akiwa hana chochote nikamlea kama mwanangu na amekuwa mwanangu, mimi na yeye tuliibadilisha gemu ya rap Marekani…<<<Birdman.
>>> Nilishawahi kumpatia Lil Wayne mkataba wa zaidi ya dola milioni 100 na kutanguliza dola milioni 67 za advance na mpaka leo huo ndio mkataba wa bei juu zaidi kwenye hii industry…sasa sielewi haya maneno yanatoka wapi lakini kama nilivyosema Wayne ni mtoto wangu atakachokifanya nitamsupport.<<< Birdman
>>> Sitaki aondoke, lakini mpaka sasa sijasikia kauli yoyote ya yeye kutaka kuondoka ikitoka mdomoni mwake, akinifuata na kusema baba nahisi umefika wakati wa mimi kufanya yangu nitamruhusu, awe au asiwe na mimi yule ni mwanangu na nitamsupport kwa kila kitu. <<<Birdman

Badaae walitoka ndani na kumalizia interview yao nje ya boti huku wakienjoy upepo mzuri wa bahari jijini Miami.
>>> “Lil Wayne akitaka kuondoka sawa nitamsupport, siwezi kumtema kisa kaachana na mimi, kama baba haitakuwa sawa kumfanyia hivyo mwanangu… Kuhusu Nicki Minaj na Drake,hapana wale hawataondoka na Wayne, Wayne kuondoka haimanishi na wao wataondoka”. <<<Birdman.
>>> “Sijui kilichotokea siku ile, mimi sikuepo mjini siku hiyo na nilisikia kuwa basi la Lil Wayne lilipigwa rasasi, na nataka ujue kitu… mtu yoyote akijaribu kumtishia Lil Wayne maisha basi amini mimi na huyo mtu tutakuwa na matatizo makubwa, lakini mimi kupanga kumuua ni kitu cha kijinga“. <<<Birdman.
Kuhusu kumwagia Lil Wayne pombe, Birdman alisema kuwa yeye hawezi kumfanyia hivyo mwanae na kwanza hawezi kufanya hivyo kwa mtu yoyote.
Hapa chini ipo exclusive interview nzima ya Birdman na Angie Martinez.






Post a Comment