Upinzani
unaokuzwa na mashabiki kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba kwenye
mitandao ya kijamii umepelekea Mastaa wa Tanzania kuanza kujitokeza
hadharani na kuwaweka mashabiki hawa sawa kwa kuamini wamevuka mipaka
kwenye ushabiki.
Mtangazaji wa TV show ya Mkasi Salama Jabir na msanii mkongwe bongoflevani Solo Thang ni miongoni mwa waliozipaza sauti zao June 30 2015.
Kupitia kwenye ukurasa wa twitter Salama Jabir aliandika ‘Wabongo
tumekua wakosoaji mpaka wasanii wanajishtukia, hakuna “zuri kabisa”
kwenye macho yetu… tuwaache wasanii wawe “Wasanii” nadhani!
‘Jana
tulikua tunaongea na wana job, Ali Kiba hakuwa mtu wa vioo vikali, yeye
alikuwa anatoa audio kali na video ya Mwananchi kamaliza, zama
zimebadilika mpaka anakwea pipa kwenda kutoa kideo kikaaali tushukuru,
kapendeza, rangi nzuri! mengine tuyaache..’ kauli ya Salama Jabiri

Post a Comment