0


Na  Gordon Kalulunga
NINI maana ya uchumi wa gesi asilia? Hilo ndilo swali nililoanza kumuuliza aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini aliyejiuzulu, Prof. Sospeter Muhongo.

Prof. Muhongo; Maana na lengo kuu na muhimu la kuingia ndani ya Uchumi wa Gesi Asilia (Gas Economy) ni kuitumia raslimali yetu ya Gesi Asilia kwa ajili ya kukuza uchumi kwa kasi kubwa na kwa kiwango kikubwa tukielekea kwenye lengo letu kuu na la msingi la kutokomeza umaskini, na nchi yetu (Tanzania) iwe ya kipato cha kati ifikapo Mwaka 2025.

Mwandishi; Gesi asilia inaweza kutumikaje?

Prof. Muhongo; Matumizi ya Gesi Asilia ni mengi. Matumizi makuu kwa upande wetu (Tanzania): 
(1) uzalishaji wa umeme wa kufikia MW 3,000 ndani ya miaka mitatu, 
(2) chanzo cha moto (heat) viwandani (k.m. viwanda vya saruji na chuma) badala ya kuni na umeme wa gharama kubwa, 
(3) kupikia - majumbani, hotelini, migahawa, mashuleni, n.k., badala ya kuni na mkaa;
(4) kutengeneza mbolea,
(5) kwenye magari,
(6) viwanda vya plastiki, 
(7)kuzalisha methanol (inayo matumizi mengi sana, k.m.  tengenezaji wa rangi, vitu vya mbao, vifaa vya plastiki; kuendesha magari na ndege, hutumika kwenye camping stoves, na waste water treatment); and other petrochemical industries, 
(8) kuuza Gesi Asilia nje ya nchi (LNG=liquefied natural gas).

Kwa hiyo Uchumi wa Gesi Asilia ndiyo Injini kuu ya kuleta  mapinduzi kwenye uzalishaji ndani ya sekta nyingine za uchumi – kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii na viwanda.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa letu, tutakuwa na uhakika wa kupata:
 (i) Raslimali Fedha, 
(ii) Vituo (centres) na taasisi za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na
(iii) Raslimali watu wenye elimu na taaluma zinazohitajika kufanya Mapinduzi ya Uzalishaji kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, na viwandani.
 
 Uchumi utakua kutoka 7% hadi zaidi ya 10% - matokeo yake ni Taifa kuwa na uchumi mkubwa na imara.

Ninamaanisha kuwa, kutokana na gesi asilia, Taifa litajitegemea na kujipangia Maendeleo yake lenyewe na kujipatia ajira mpya kwa wingi kwnye sekta zote za uchumi.

Mwandishi; Mbali na Tanzania kuna nchi zingine zenye gesi asilia na zinauzaje?

Prof. Muhongo; Ndiyo zipo na zenye gesi hizo zaidi hazizidi kumi ambazo ni Russia (1, 720 trillion cubic feet, tcf/ GDP per capita – US$ 12,925), Iran (1,187 tcf/US$ 5,183 ), Qatar (885 tcf/ US$ 93,965), Turkmenistan (618 tcf/US$ 8,270), USA (348 tcf/US$ 54,596), Saudi Arabia (304 tcf/US$ 24,454), Iraq (226 tcf/US$ 6,164), Venezuela (202 tcf/US$ 6,756),  Nigeria (180 tcf/US$ 3,298) na Algeria (159 tcf/US$ 5,531).

Mwandishi; Kuna mahitaji makubwa ya gesi asilia duniani?

Prof. Muhongo; Mwaka 2013, mahitaji (demand) ya Gesi Asilia Duniani yalikuwa takribani mita za ujazo trilioni 3.50 (sawa na 123.6 tcf).

Inaonekana kwamba mahitaji ya Gesi Asilia Duniani yanazidi kuongezeka na ifikapo Mwaka 2019 mahitaji yatafikia mita za ujazo trilioni 3.98 (140.6 tcf), na ifikapo Mwaka 2020 mahitaji yatavuka mita za ujazo trilioni 4 (141.3 tcf) – Gas is on its way to cross the 4, 000 bcm mark by 2020.

International Energy Agency (IEA, 2014) inakisia kwamba mahitaji ya nishati Duniani yataongezeka kwa 37% ifikapo Mwaka 2040, na vyanzo vikuu vya nishati vitakuwa ni mafuta (oil), gesi asilia (gas), makaa ya mawe (coal) na vyanzo vingine vyenye carbon kidogo (low-carbon sources). IEA inakadiria takribani Giga Watt (GW) 7,200 zitahitajika ili kuendana na mahitaji ya nishati Duniani ifikapo Mwaka 2040.

Japokuwa nishati ya nuklia (global nuclear power capacity) itaongezeka kwa 60%, kutoka GW 392 Mwaka 2013 hadi GW 620 Mwaka 2040, bado mitambo takribani 200 (nuclear reactors) kati ya 434 iliyokuwa inafanya kazi kufikia Desemba 2013 (ipo Europe, USA, Russia na Japan), itafungwa ifikapo Mwaka 2040. Kwa hiyo mahitaji ya Gesi Asilia yatakuwa makubwa kuziba  pungufu utakaotokana na mapengo ya nishati ya nuklia, n.k.

Gesi Asilia itahitajika Duniani kote kuliko vyanzo vingine vya nishati (fossil fuels).

Mahitaji makubwa Duniani (2040) ya Gesi Asilia yatakuwa ni kuzalisha umeme (37%). Kwa bahati nzuri Tanzania tunayo Gesi Asilia nyingi na makaa ya mawe kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na matumizi mengine.

Wenzetu wameweza kwa nini Tanzania yenye 55.08 tcf (April 2015) ishindwe? Kuna uhakika wa mashapo (reserves) kuongezeka, hasa kwenye blocks zetu za Kusini, karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji; na zile za Kaskazini.

Tukiendelea kutafuta Gesi Asilia na LNG na Mafuta kwa umakini na utulivu mkubwa, tutavuka mashapo (reserves) ya 100 tcf miaka michache sana ijayo.

Mwandishi; Prof. Muhongo, Mtanzania wa kawaida anaweza kufahamu vipi na kuelewa unapozungumzia suala la Gesi asilia hasa LNG?

Prof. Muhongo; LNG ni Gesi Asilia (predominantly methane) iliyogeuzwa kuwa kimiminika (liquid) kwa kupozwa hadi nyuzi 162 chini ya zero (-162ºC) kwa sababu ya kurahisisha utunzaji (storage) na usafirishaji (transport).

Kampuni ya SHELL imebashiri kwamba mahitaji ya LNG yataongezeka kwa kiasi cha 5% kwa mwaka, ikiwa ni 16% ya jumla ya mahitaji 2011 mahitaji ya LNG yalikuwa takribani tani milioni 250,  Mwaka 2020 na ifikapo Mwaka 2025 milioni 500.

Asia na Mashariki ya Kati zitaongoza kwa kuwa na mahitaji makubwa. Kwa sasa Qatar ndiyo nchi inayozalisha LNG nyingi Duniani. Angola ilianza uzalishaji Mwaka 2013. 

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Post a Comment

 
Top