Hemed alitweet
kwamba jina lake halipo kwenye list ya wasanii wanaoshiriki Tuzo za
Shirikisho la Filamu TZ, leo katafutwa Rais wa Shirikisho hilo,
Mwakifwamba ambae amesema walitangaza sana kuhusu ishu ya wasanii
kupeleka kazi zao ili ziingizwe kwenye Tuzo hizo lakini wasanii wengi
hawakufanya hivyo.
Dully Sykes karudi
tena, amegoma kabsa kwani kupanda tena ndege?? Jibu ni hapana !! Dully
kasema alikuwa na uoga sana kusafiri na ndege kwa kuwa alihofia kifo cha
ajali, lakini akashuhudia msiba wa baba yake mzazi akaona kumbe kifo
kiko sehemu yoyote.. kwa sasa yuko tayari kuendelea kutumia usafiri wa
ndege, hana sababu ya kuendelea kuogopa.
Rapper Mabeste
amesema kwamba kaandaa show ambayo itafanyika Club Maisha siku ya
Jumapili kwa ajili ya kukusanya pesa ambazo zitamsaidia matibabu ya
mkewe ambaye ni mgonjwa kwa kipndi kirefu sana.
Mabeste
amesema kuhusu kiasi cha pesa ambacho kinatakiwa kwa ajili ya matibabu
hawezi kukitaja kwa kuwa gharama ziko kwenye kila hatua, kakaa bila
kufanya kazi kwa muda mrefu kwa kuwa alikuwa akimuuguza mke wake, hakuna
mtu mwingine ambaye alitoa msaada kuuguza wala kumlea mtoto wao ambae
ni mdogo.
Cha mwisho kinahusu Tuzo za KTMA.. msanii Mo Music amesema hakuagiza mtu yeyote kwenda kumchukulia cheti cha BASATA kwa kuwa yeye alitangaza kujitoa kushiriki Tuzo za KTMA mwaka huu 2015.. Mo
kasema kwa kuwa picha za mtu huyo zipo inatakiwa BASATA wafanye
utaratibu wa kumtafuta ili aeleze kwa nini kajitambulisha kumuwakilisha
msanii huyo wakati yeye hakumuagiza



Post a Comment